27 Septemba 2025 - 11:40
Source: ABNA
Hotuba ya Netanyahu kwa Viti Vilivyoachwa Wazi vya Umoja wa Mataifa!

Gazeti la lugha ya Kiebrania limejibu hotuba ya Netanyahu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa mbele ya viti vilivyoachwa wazi.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la AhlulBayt (ABNA), gazeti la lugha ya Kiebrania "Yedioth Ahronoth" lilikiri kwamba kuondoka kwa wakuu wa nchi kutoka ukumbi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa kuanza kwa hotuba ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, kulionyesha kwa njia dhahiri kabisa ni kwa kiasi gani utawala huu umetengwa na ulimwengu leo.

Jana usiku, wakati huo huo na kuanza kwa hotuba ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, viongozi na wakuu wa nchi duniani walimzomea na hotuba yake ilianza katika dakika za kwanza kwa kelele kubwa za waliohudhuria.

Pamoja na kuanza kwa hotuba ya Netanyahu, baadhi ya wakuu na viongozi wa nchi duniani walitoka ukumbini mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Barak Ravid, mwandishi wa Kizayuni wa tovuti ya Axios, alichapisha picha inayoonyesha wakuu na marais wa nchi duniani wakiondoka mwanzoni mwa hotuba ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, na kutangaza: Ukumbi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa sasa uko wazi.

Wakati huo huo na hotuba ya Netanyahu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wananchi wa Marekani walifanya maandamano makubwa mbele ya jengo la Umoja wa Mataifa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha